Kidato cha sita Waliochaguliwa Kujiunga NA JKT 2016

Matangazo
Matangazo

Kidato cha sita waliochaguliwa kujiunga na jkt 2016, Form six selected to join jkt 2016, Vijana wa kidato cha sita waliochaguliwa kujiunga na jkt 2016, jkt 2016, mufunzo ya jkt 2016, kujiunga na jkt Tanzania 2016. 


Kidato cha sita Waliochaguliwa Kujiunga NA JKT 2016


KIDATO CHA SITA (FORM SIX) KUJIUNGA NA JKT 2016

TANGAZO MUHIMU KWA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA MEI 2016

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita (Form six) kwa mwaka 2016, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 - 05 Juni 2016.
Vijana waliochaguliwa, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.

Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti Kambi ya JKT RUVU, iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

JKT linawataka vijana hao kuripoti makambini wakiwa na nguo za michezo kama vile ‘track suit’, bukta, raba pamoja na nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa kwenye makambi yenye baridi kama JKT Makutupora, JKT Mafinga, JKT Mlale, JKT Kanembwa na JKT Mtabila.
Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochanguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, uhodari, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.  

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 20 Mei 2016


TANGAZO

MABADILIKO YA TAREHE YA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2016.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linautangazia umma mabadiliko ya tarehe ya kuripoti makambini vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2016 na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2016.

Taarifa ya awali kwa vyombo vya habari nchini ilianisha tarehe ya kuripoti kuwa ni tarehe 01 June hadi tarehe 05 Juni 2016. Tarehe hiyo imeafanyiwa mabadiliko badala yake vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 07 June hadi tarehe 10 June 2016 bila kukosa.

Atakayesikia tangazo hili amtaarifu na mwezie.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 31 Mei 2016


Vikosi Walivyopangiwa Vijana kwa mujibu wa Sheria 2016 - KIDATO CHA SITA (FORM SIX) WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT 2016.

Artikel Terkait